Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga Moro wafanya usafi, Zahera atoa dola 1000

Wed, 31 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

WANACHAMA  na mashabiki waYanga wamefanya usafi katika hospitali ya mkoa asubuhi hii.

Wanachama hao wa Mkoa wa Morogoro wamefanya usafi huo katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ikiwa ni moja ya kazi zinazofanyika kuelekea kilele cha wiki ya Mwananchi Agosti 4.

Wakiongozwa wajumbe wao wa kamati ya utendaji ya Yanga Mhandisi Bahati Mwaseba na Hamad Islam mbali na kufanya usafi pia waligawa vitu mbalimbali.

Zoezi hilo pia liliwahusisha kocha mkuu Mwinyi Zahera na wasaidizi wake Noel Mwandila na mratibu wa timu hiyo Hafidh Saleh.

Katika jukumu hilo kocha Zahera alitoa kiasi cha dola 1000 (sh 2.2 milioni)akiwakabidhi wakinamama waliojifungua wodini.

Zahera amesema hatua ya hospitali hiyo kuwapokea katika kazi hiyo imemfanya kutoa kiasi hicho cha fedha kwa wakinamama hao waliojifungua.

Chanzo: mwananchi.co.tz