Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga, Mayele wote kileleni Ligi Kuu NBC

Fiston Kalala Mayeleee.jpeg Kinara wa upachikaji mabao Ligi Kuu, Fiston Mayele

Sun, 27 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Klabu ya Yanga ikiendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu NBC hapo jana kwa kuichapa klabu ya Mbeya City mabao 2-0 na kufikisha alama 32.

Mshambuliaji hatari wa timu hiyo Fiston Mayele nae hajabaki nyuma kwani anaendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kunyakua kiatu cha mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2022/23.

Mayele ambae aliweka wazi masikitiko yake ya kukosa kiatu cha mfungaji bora msimu uliopita mbele ya mzawa George mpole, anaonekana kujizatiti hasa msimu huu kuhakikisha anaondoka na zawadi hiyo kwa kujitahidi kufunga mabao kwa kadri anavyopata nafasi.

Mpaka sasa Mayele ndio kinara wa upachikaji mabao akiwa na magoli 10 akifuatiwa na mshambuliaji wa Mbeya City Sixtus Sabilo mwenye mabao 7.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live