Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Malengo yetu sasa ni mpaka fainali CAFCL

Yanga Gamondi Wachezaji Yanga: Malengo yetu sasa ni mpaka fainali CAFCL

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imesema kuwa, malengo yao kwa sasa ni kucheza fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, hivyo wapo tayari kukutana na timu yoyote mbele yao kwenye hatua ya mtoano.

Hayo yamesemwa leo na Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe wakati akizungumza na wanahabari leo kuelekea mchezo wao wa mwisho kwenye hatua ya makundi dhidi ya Al Ahly, mchezo utakaoipigwa Ijumaa, Machi 1, 2024 nchini Misri.

Itakumbukwa kuwa, mwanzoni mwa msimu, Yanga ilieleza kuwa licha ya kucheza fainali ya CAFCC msimu uliopita, malengo yao ya msimu huu yalikuwa kufika hatua ya makundi ya CAFCL lakini wanaona ipo nafasi ya kufanya makubwa zaidi hasa baada ya kufanikiwa kutinga robo fainali ya michuano hiyo kwa kuifunga CR Belouizdad kwa bao 4-0, Jumamosi iliyopita.

“Wakati tunaanza michuano ya CAFCL, uongozi wa Yanga ulinituma nije niwaambie Watanzania kuwa lengo la yanga kwenye michuano hii ni kufika hatua ya makundi, niliwaeleza na baada ya hapo mkaanzisha mijadala kwenye radio, Tv na mitandaoni kwamba yanga ni waoga, malengo madogo timu kubwa, mara hatutoboi, sisi tukasimamia maengo yetu na tukatoboa.

“Baada ya kufika makundi mlitaka tujitoe kwa sababu tumetimiza malengo yetu? Baada ya kufika pale tulifanya utafiti kwanza tukaangalia kundi lenyewe, jeografia, na mazingira yote na nikaja kuwaambia kuwa tunakwenda kuwaonyesha Yanga tuna nini na kuna chances za yanga kwenda robo fainali kwa vile tunaheshimu Al Ahly na CR Belouizdad.

“Hapa tumeuza brand ya timu yetu kwa sababu lilikuwa kundi gumu, Afrika nzima wametujua mpaka Waarabu na ukubwa wao wamekunjana mashati wapigane sababu ya soka la Yanga na sio hujuma nje ya uwanja. Mpira wa Yanga ulishahama mdomoni unapigwa mguuni.

“Baada ya kufika robo sasa niwaambie Wanayanga kwamba tundu tulilolitaka tumetumbukia, na tupo kwenye knockout stage, nipige kwako nikupige kwangu. Malengo yetu sasa sio kuanza kupiga hesabu vipi bali kwenda mpaka mwisho wa wa michuano hii panapo majaliwa na Mwenyezi Mungu.

“hatujui mbele anakuja nani lakini anayekuja ajue kabisa kwamba ana dakika 90 kwake na 90 kwetu, na sisi Yanga tunayo quality ya kucheza mechi mbili za nyumbani na ugenini," amesema Ally Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live