Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Kwa balaa hili, tutatikisa Afrika

Tu Gamondi Zs Yanga: Kwa balaa hili, tutatikisa Afrika

Thu, 11 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya misimu miwili mfululizo iliyopita 2022-2023 na 2023-2024 kikosi cha Young Africans kuitikisa Afrika kutokana na kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa, Kocha Mkuu Miguel Gamondi amesema tunakwenda kufanya hivyo tena.

Gamondi amepata jeuri ya kusema baada ya kuona maboresho ya kikosi yalivyofanyika kulingana na malengo yaliyopo. Ikumbukwe kwamba katika misimu miwili mfululizo 2022-2023 na 2023-2024 Young Africans tumeitikisa Afrika kufanya vizuri michuano ya kimataifa.

Msimu wa 2022-2023 Yanga ilicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kisha 2023-2024 ikacheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku msimu ujao 2024-2025 ambao itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika malengo ni kufika mbali zaidi ikiwemo fainali na kubeba ubingwa.

“Malengo yetu kwa pamoja kama klabu chini ya Rais Eng Hersi Said ni kuunda timu ya kutikisa Afrika.

“Hilo nimeliona linakwenda kutimia kutokana na namna kikosi cha sasa kilivyofanyiwa maboresho ya kuingiza wachezaji wapya na wale wa zamani kuboreshewa mikataba yao,” alisema Gamondi.

Katika maboresho yaliyofanyika, wachezaji ambao mikataba yao imemalizika na kuwepo katika mipango ya benchi la ufundi wameongezewa.

Wachezaji hao ni Aboutwalib Mshery, Djigui Diarra, Kibwana Shomari, Nickson Kibabage, Bakari Mwamnyeto, Farid Mussa na Stephane Aziz Ki.

Mbali na hao, kuna maingizo mapya ya wachezaji watano ambao ni Clatous Chama, Prince Dube, Chadrack Boka, Khumeiny Aboubakar na Aziz Andambwile.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live