Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Kisasi kimelipwa lakini bado hatujamalizana

Arafat Haji Kisasi Makamu wa Rais Klabu ya Yanga, Arafat Haji

Tue, 25 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais wa Yanga, Arafat Ally Haji amenunua tiketi 500 za kushuhudia mchezo wetu wa robo fainali #cafconfederationcup dhidi ya Rivers United, kwa wote watakaojitokeza kwenye zoezi la uchangiaji damu litakalofanyika siku ya Ijumaa tarehe 28 katika viwanja wa Leaders Club, Dar Es Salaam.

Uongozi wa Yanga unayakaribisha Makampuni/Taasisi mengine kununua tiketi kwa ajili ya kuwazawadia mashujaa wote watakaojitolea damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya wengine.

Yanga wanatumia mchezo huo kuhamasisha wananchi kuchangia damu huku wakienda na kauli mbiu yao kuwa "kisasi kimelipwa lakini bado hatujamalizana".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live