Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Kimataifa bado

Hersi Said.png?fit=640%2C420&ssl=1 Yanga: Kimataifa bado

Thu, 14 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Hersi Said amesema kwamba licha ya baadhi ya watu kuanza kuipigia hesabu michuano ya kimataifa msimu ujao, hilo kwasasa sio kipaumbele chao bali wanachokiwaza ni kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara.

Hersi ambaye ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM amesema kuwa mara zote yeye huwa anafikiria kilicho mbele yake na anachofahamu ni kwamba wana Yanga wote wana kiu ya kutwaa Ubingwa wa NBC.

''Kama nilivyosema awali ni kuwa tulikuwa tunaijenga klabu yetu ili tufanikiwe kwenye mashindano ya ndani, ukishalifanikisha hilo ndipo tutaweza kupambana kwenye michuano ya kimataifa na hilo lipo katika mipango yetu'' Hersi Said Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM.

Katika hatua nyingine Hersi amesema wanajiandaa kwa ajil ya kuwakabili watani zao wa jadi Simba katika mchezo wa tarehe 30 ambao utatoa taswira pana juu ya safari yao ya ubingwa msimu huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live