Dakika 45 za kipindi cha kwanza katika mchezo wa Yanga na KMC mchezo huo hakuna ambaye ameonyesha ubabe kwa mwenzake kwa kuweka mpira wavuni.
Licha ya matokeo hayo KMC imeonyesha ubora wa kutengeneza nafasi nyingi lakini utulivu kwenye umaliziaji ni changamoto.
Katika kipindi cha kwanza timu zote zilianza kucheza kwa kuviziana huku wakitumia zaidi upande wa pembeni.
Yanga ilikuwa inatumia zaidi upande wa kulia ambao alikuwa anacheza Tuisila Kisinda lakini mchezaji huyo alikuwa hawezi kupenya safu ya ulinzi ya KMC upande wa kushoto aliokuwa anacheza Hance Masoud.
Upande wa KMC wao walikuwa wanatumia winga zote mbili kulia ikiwa na beki Kelvin Kijiri ambaye alikuwa na uwezo wa kupeleka mashambulizi langoni kwa Yanga lakini na yeye utulivu alikosa.
Upande wa kushoto KMC ilikuwa inamtumia George Makang’a ambaye alikuwa na uwezo wa kumiliki mpirwbna chenga zilizokuwa zinamuweka kwenye wakati mgumu Dickson Job wa Yanga.
Dakika ya 5 Aziz Ki wa Yanga alitaka kuiandikia bao la kuongoz timu yake baada ya kupiga faulo iliyoenda moja kwa moja langoni lakini kipa wa KMC, David Kissu aliucheza mpira na kuwa kona isiyo na faida.
Faulo hiyo ilitokana na Heritier Makambo wa Yanga kufanyiwa madhambi na Ibrahim Ame wa KMC.
Dakika ya 37 KMC ilitaka kuandika bao la kuongoza baada ya Matheo Anthony kukimbia na mpira
Dakika ya 39 KMC ilifanya shambulizi lingine baada ya Kelvin Kijiri kupiga krosi lakini washambuliaji wake Matheo Anthony na Emmanuel Mvuyekure waligongana na kuupiga mpira kichwa ukienda nje.
Dakika ya 43 winga wa Yanga, Dickson Ambundo alionyeshewa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi George Makang’a.
Dakika ya 44 KMC ilikosa bao la wazi baada ya Hance Masoud kupiga pasi ya haraka kwa George Makang’a ambaye aliingia na mpira ndani ya boksi na kupiga pasi ya chini lakini Matheo Anthony alichelewa kuucheza na kutoka nje.
Yanga nao walijibu mapigo dakika ya 45 baada ya Gael Bigirimana kupiga pasi ya juu juu na Heritier Makambo aliiunganisha kwa kichwa mpira ukiyoka nje kidogo ya goli.