Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Ishu ya ubingwa imeisha hiyo

Yanga Kikosii Ofisa habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe.

Sat, 11 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, wamesema nia yao ni kutangaza ubingwa Mei 22, wakiwa Makao Makuu ya nchi, jijini Dodoma watakapocheza dhidi ya Dodoma Jiji kwenye uwanja wa Jamhuri.

Yanga imebakisha michezo minne ambapo katika hiyo itaanza kucheza na Mtibwa Sugar keshokutwa Manungu na baadae kwenda Dodoma kucheza na Dodoma jiji huku ikisaka pointi nne tu kuweza kutangaza ubingwa.

Ofisa habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe, amesema ingawa kwa sasa ligi imekuwa ngumu sana kwa kipindi hiki ambacho inaelekea ukingoni, watafanya kila njia kuhakikisha wanashinda mechi mbili zijazo ili watangaze ubingwa wakiwa Makao Makuu, Dodoma.

"Mechi za mwisho zina presha yake na ugumu wake,tunatarajia kupata ushindani mkubwa, ila sasa tumekaa vizuri kabisa, ukipiga mahesabu bado pointi nne hivi kuweza kuwa mabingwa, kwa hiyo niwaambie wanachama na mashabiki wetu kazi bado inaendelea, tuna mechi mbili dhidi ya Mtibwa Sugar na Dodoma Jiji, kama tukishinda hizi, basi ubingwa tutautangazia Dodoma," alisema Kamwe.

Endapo Yanga itashinda mechi yake ya Jumatatu dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Manungu Complex, Turiani, Morogoro, itahitaji sare tu dhidi ya Dodoma Jiji ili kutawazwa kuwa wafalme wa nchi kwa mara ya tatu mfululizo.

Kama matokeo yatakuwa tofauti katika michezo hiyo miwili, basi Yanga itawabidi wasubiri mechi zingine mbili zinazofuata ili kuona uwezekano wa kutangazwa mabingwa kwa mara ya tatu mfululizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live