Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga Gamondi kukipiga na Kaizer Chiefs ya Nabi Kombe la Toyota

Video Archive
Mon, 8 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Young Africans imepata mwaliko wa kucheza mchezo maalum wa Kombe la Toyota dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Mchezo huo umepangwa kuchezwa Julai 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Toyota uliopo Bloemfontein nchini Afrika Kusini.

Kwa sasa Kaizer Chief inafundishwa na Kocha Nasreddine Nabi raia wa Tunisia aliyewahi kuitumikia Yanga na kuipa mafanikio makubwa ikiwa ni ubingwa wa Ligi mara mbili, Shirikisho mara mbili, ngao ya Jamii mara mbili na kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kuifanya yanga kuwa tishio katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kabla kutimkia AS FAR Rabat ya Morocco msimu uliopita lakini hivi karibuni ameondoka na kujiunga na Kaizer ambao wamekuwa wakimuwinda tangu akiwa Yanga.

Taarifa iliyotolewa na Kaizer Chiefs, imeeleza kwamba: “Kaizer Chiefs watakuwa wenyeji wa Young Africans katika mchuano wa kwanza wa Kombe la Toyota utakaochezwa kwenye Uwanja wa Toyota mjini Bloemfontein mnamo tarehe 28 Julai 2024.”

Rais wa Young Africans, Eng. Hersi Said, amezungumzia mwaliko huo kwa kusema: “Kama Young Africans SC, tunafurahishwa sana na mwaliko huu wa kushiriki katika Kombe la Toyota 2024.

“Mchezo huu unaendeleza uhusiano kati ya timu zetu kubwa mbili barani Afrika ambao ulianza mwaka jana tulipowaalika Kaizer Chiefs kushiriki katika Tamasha la Wiki ya Mwananchi. Tunafurahia mwaliko huu na tunaahidi kutoa mchezo wa ushindani utakaotusaidia kujiandaa kwa msimu mpya wa 2024/25.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live