Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema kuwa kiungo wao mshambuliaji, Feisal Salum Abdallah 'Fei Toto' hajawahi kuwa na changamoto ya kinidhamu tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2018.
Hersi amesema hayo wakati akihojiwa na moja ya media nchini Tanzania kufuatia sakata la mchezaji huyo kuomba kuvunja mkataba ili aondoke klabuni hapo.
“Feisal ni mmoja kati ya Wachezaji bora na wenye nidhamu ambao tumewahi kuwa nao Yanga hadi leo katika Wachezaji ambao niliwakuta Yanga, yeye ni mchezaji mkongwe zaidi kati ya wote sababu hakuna yeyote aliyesalia Yanga hadi leo ispokuwa yeye, lakini pia hajawahi kuwa na changamoto yoyote ya kinidhamu, alikuja akiwa mdogo ndio maana akapewa jina la Fei Toto.
“Kama GSM tuliwahi kumwita Feisal na kukaanae kujadili maslahi yake ambayo hayakuwa madogo hata kwa wakati huo, alikuwa akipokea mshahara wa Tsh 1.5m na tukamuongezea hadi kufikia Tsh Million 4 kwa mwezi pamoja na signing fee ya Tsh Million 100, kuna Watu wanauliza kuhusu maslahi ya Feisal ikiwa sisi tuliyaboresha tangu mwaka 2020.
“Sitaki kwenda mbali ila mimi naamini kuna kitu nyuma ya Feisal kinachomsukuma kufanya haya,” -Engineer Hersi Said @caamil_88 Rais wa Klabu ya @yangasc akizungumza kwenye #PowerBreakfast ya CloudsFM.