Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga, Chivaviro sasa kimeeleweka

Ranga Chivavirojangwani Ranga Chivaviro.

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya dirisha dogo la usajili Tanzania Bara kufunguliwa, mabosi wa Klabu ya Yanga wamefikia hatua nzuri ya mazungumzo na uongozi wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini juu ya uwezekano wa kuinasa saini ya mshambuliaji wa timu hiyo, Ranga Chivaviro, imefahamika.

Yanga imekuwa ikitafuta mbadala wa Fiston Mayele aliyetimkia Misri katika Klabu ya Pyramid ambapo nafasi yake ilitarajiwa kuzibwa na Hafiz Konkoni, ambaye hata hivyo ameshindwa kuonesha makali yake ndani ya kikosi hicho hali iliyosababisha klabu hiyo kuelekeza nguvu zao katika kuisaka saini ya Chivaviro mwenye umri wa miaka 31.

Hata hivyo, licha ya uongozi wa juu wa klabu hiyo kuweka bayana kuwa suala la usajili ndani ya timu hiyo kwa sasa lipo chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi, lakini Nipashe limefahamishwa kwamba tayari mabosi wa timu hiyo wamekuwa na mawasiliano mazuri na viongozi wa Kaizer Chiefs juu ya uwezekano wa kumnunua mshambuliaji huyo ama kumpata kwa mkopo.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo kimeliambia Nipashe kuwa kwa sasa wapo katika mazungumzo ya kuona wanalimaza vipi na kumpata mshambuliaji huyo wa kati raia wa Afrika Kusini.

"Ni kweli tumekuwa na mazungumzo na viongozi wa timu ambayo anacheza huyo mchezaji kwa sababu bado nafasi ya mshambuliaji wa kati imekuwa tatizo na huyo mtu tunaona anaweza kutusaidia katika eneo ambalo tumeshindwa kupata dawa, kama kila kitu kikienda sawa basi tunategemea kuwa naye hapa," alisema mtoa taarifa wetu.

Mtoa habari huyo alisema baada ya kufikia mapendekezo hayo, viongozi kupitia rais wa klabu hiyo, Hersi Said, alikuwapo Afrika Kusini kuzungumza na Kaizer Chiefs kwa ajili ya kuinasa saini ya nyota huyo.

"Kwa sasa hatua mshambuliaji mzoefu halisia na Kocha Gamondi amewataka viongozi kuanza na jambo hilo na tayari Hersi alifanya kikao na viongozi wa Kaizer Chiefs kwa ajili ya kumalizana na Chivaviro.

"Kikao hicho kimeenda vizuri na sasa imebaki hatua chache, ila haijafahamika vizuri ukubwa wa mkataba wake aliomalizana na Yanga na muda atakaojiunga nao kambini, ila taarifa za uhakika ni kwamba Chivaviro atakuwa miongoni mwa nyota atakayecheza Yanga," alisema.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe, zoezi la usajili wa dirisha dogo wameshakamilisha na sasa wanasubiri kazi ya kutambulisha.

Alisema Kocha Gamondi tayari amekabidhi ripoti na tayari imeshafanyiwa kazi kwa kusajili mchezaji ambaye atakuja kuwa msaada kwenye timu ikiwamo safu yao ya ushambuliaji ambayo imefanyiwa kazi.

“Ni kweli tutafanya usajili kulingana na mapendekezo ambayo ameyaomba Gamondi, tayari kazi imefanyika, kwa rais wetu, Hersi kufanya kazi ya usajili mapema sana na tutashusha mtu hatari ambaye atakuja kukata kiu cha mashabiki wetu,” alisema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: