Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga Bingwa Ngao ya Jamii 2024

Yanga Bingwa Ngao Ya Jamii.jpeg Yanga Bingwa Ngao ya Jamii 2024

Sun, 11 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Timu ya Yanga imebeba Ngao ya Jamii 2024 kwa ushindi mnono wa magoli 4-1 dhidi ya AzamFC kwenye Uwanja wa Mkapa katika Fainali ya Michuano hiyo, leo Agosti 11, 2024

Feisal Salum “FeiToto” ndiye aliyeanza kufunga upande wa Azam FC lakini Yanga ikasawazisha kupitia kwa Prince Dube na kuendelea kuongeza magoli mengine kupitia kwa Yoro Diaby (amejifunga), Stephane Aziz Ki na Clement Mzize

Yanga iliingia Fainali hiyo kwa kuifunga Simba goli 1-0 wakati Azam FC iliifunga Coastal Union magoli 5-2.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: