Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga, Belouidad ni dakika 60 tu!

Yanga Cr Belouizdad WA0002 Yanga vs Belouidad.

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Pambano la Kundi D la Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na CR Belouidad ya Algeria limepigwa kwa muda wa dakika 60 tu uwanjani, huku nyingine zilipotea kwa matukio tofauti, lakini kitu muhimu kwa mashabiki wa wenyeji ni chama lao kutinga robo fainali kibabe kwa kuwazamisha Waarabu kwa mabao 4-0.

Ushindi wa juzi ulikuwa ni mkubwa kwa timu zote katika hatua ya makundi hadi sasa, lakini wa kwanza kwa Yanga ikiwa timu ya kwanza ya Tanzania kushinda idadi kama hiyo dhidi ya timu za Kaskazini maarufu kama Waarabu na kutinga robo ikiwa bado ina mchezo mmoja mkononi.

Usichokijua ni mchezo huo ulipigwa kwa muda wa dakika 60, nyingine zilipotea kwa matukio mbalimbali kama Mwanaspoti ilivyoweza kuufuatilia mwanzo mwisho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa mchezo huo uliokuwa ni mtoko wa Pacome ambapo mashabiki, viongozi na baadhi ya wachezaji kupata rangi nywele ili wajifananishe na Pacomer Zouzoua.

DAKIKA 60 Mechi hiyo ilipaswa kuchezwa kwa dakika 90, lakini ukweli ni zilitumika dakika 60 pekee baada ya kuchezwa kwa saa 1:00:30:58 huku mwamuzi Boubou Traore kutoka Mali kuongeza dakika nne pekee za kufidia muda uliopotezwa kwa matukio hasa katika kipindi cha kwanza.

Belouzdad ilikuwa na matukio mengi ya kupoteza muda hasa kipindi cha kwanza yaliyomfanya Traore kushtukia mbinu zao na kuwa mkali na kupuuza matukio yao ya kujiangusha, lakini bado haikutosha kuokoa muda ambao ulipaswa kutumika kuchezwa kwenye mchezo huo.

Matukio ya mipira kutoka nje ya uwanja na kuchukua muda kurushwa au pale linapotokea tukio la kupigwa kona au frikiki kama sio golikiki, wachezaji wa timu zote walionekana kupoteza muda mbali na matukio ya wachezaji kuanguka na kuhitaji kupewa huduma za kwanza.

Huenda kama dakika 30 zilizopotezwa kwa matukio mengine yangetumika kihalali huenda matokeo ya mchezo huo yangeweza kywa mengine tofauti na 4-0 ilizopata Yanga mbele ya CRB.

PACOME FUNDI Kiungo Pacome Zouzoua ambaye mchezo huo ilikuwa kama siku yake aliikamata vizuri shoo hiyo akiwa ndiye injini ya mashambulizi mengi ya Yanga kwenye mchezo huo alikuwa na balaa zito kila alipokuwa anagusa mpira.

Zouzoua alikuwa na nguvu, kasi, mbinu na akili kubwa kila alipoanzisha mashambulizi ya timu yake na kuwaweka kwenye wakati mgumu wapinzani wao hao kwenye mchezo huo, ingawa hakufunga lakini alihusika kwa nafasi kubwa kuutengeneza ushindi huo.  

BASI LA BELOUIZDAD Yanga kushinda mabao 4-0 ni makosa yao tu lakini ingeweza kutengeneza ushindi mkubwa zaidi ya huo baada ya kutengeneza nafasi nyingi kwenye mchezo huo lakini ikazitumia nne pekee.

Belouizdad ilifanya makosa mengi ambayo yaliwafanya wenyeji kuipasua ngome yao lakini umakini wa washambuliaji wa Yanga ndio uliowaokoa Waarabu hao wasidhalilike kwa kipigo cha ajabu.

UKUTA, KIUNGO BALAA Yanga ilikuwa imara eneo la kiungo kocha wao Miguel Gamondi aliwapanga vizuri viungo wake katikati ya uwanja akimfanya Khalid Aucho atumie muda mwingi kucheza kama mkabaji huku viungo wawili wa juu wakichezesha timu lakini pia wakirudi kwa haraka chini kama timu yao inashambuliwa.

Eneo lingine ni safu ya ulinzi ambayo ilifanya kazi kubwa kuwazima wageni hasa kipindi cha pili ambacho baada ya kuruhusu mabao matatu walikuja na presha kubwa ikitafuta bao lolote ambalo lingewatibulia hesabu wenyeji.

JOTO LATESA Hakuna shaka kwamba Belouizdad iliteseka na hali ya joto la jijini Dar es Salaam, wageni hao hawakuwa na kasi iliyozoeleka kwani katika kipindi cha pili ilionekana wazito tofauti na wenyeji waliocheza wakiwa wameizoea haloi hiyo, licha ya mechi kupigwa saa 1:00 usiku.

Hali hiyo ya joto ilisababisha mwamuzi mara kadhaa kutoa muda wa mapumziko ya kama dakika mbili ili wachezaji na waamuzi kupata muda wa kupooza makoo kwa maji.

GUEDE GARI LIMEWAKA Tofauti na alivyoanza kuitumikia Yanga, kwa sasa mshambuliaji Josph Guede ni kama viole gari limewaka tangu alipofunga mabao mawili kwenye mechi ya ASFC dhidi ya Polisi Tanzania, kwani juzi aliingia uwanjani na kucheza kumpokea Kennedy Musonda na dakika 23 alizocheza zilitosha kuonyesha makali yake ya sasa.

Guede alifunga bao la nne na lililochangia kuipa Yanga tiketi ya robo fainali akimalizia pasi murua ya Stephane Aziz KI akitumia mguu wa kulia kutupia, tofauti na mabao mawili ya ASFC aliyofungwa kwa kichwa akimaliza krosi za Augustine Okrah.

Kuanza kutupia kwa Guede kulimfanya hadi kocha Miguel Gamondi kukiri kazi ndo imeanza kwa mshambuliaji huyo kutoka Ivory Coast.

“Nampongeza sana naelewa kama mchezaji alikuwa na wakati gani kucheza mechi mfululizo bila kufunga lakini bado ukaweza kuendelea. Huu ni mwanzo mzuri kwake kwani ameonyesha uwezo wake katika mechi muhimu ambayo timu ilikuwa inatakiwa kuvuna ushindi mwingi ili kutinga hatua inayofuata,naamini atafanya makubwa sana,” alisema Gamondi.

Katika dakika hizo 23 alizocheza mshambuliaji huyo zimezaa matunda, huku katika muda wote alikuwa na tachi sita, alipokonya mpira mara moja na kupokonywa mara moja pia, alifika ndani ya boksi mara moja na hapo ndipo alipofunga bao hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: