Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga, Azam vuta nikuvute Kileleni Ligi Kuu

Azam FC Kuendelea Kuchezea Kichapo Kwa Yanga Jumapili Yanga, Azam vuta nikuvute Kileleni Ligi Kuu

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ligi Kuu Bara leo inaendelea tena katika viwanja vitatu hapa jijini Dar es Salaam ambapo Yanga itaikaribisha Singida Big Stars mchezo utakaopigwa uwanja wa Mkapa saa 12:15 wakati huo huo Azam ikiikaribisha Namungo mechi itakayochezwa katika uwanja Azam Complex saa 2:30 na KMC ikicheza dhidi ya Tanzania Prisons saa 10:00 jioni katika uwanja wa Uhuru.

Katika mechi hizi za leo, Yanga na Azam ni sehemu ya mtegeano katika msimamo wa Ligi kutokana na timu zote kuwa nafasi nzuri.

Yanga ndio kinara katika msimamo akiwa na pointi 15 lakini Azam Fc inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 13 na michezo sawa na Yanga (mitano) hivyo anahitaji ushindi ili kufikisha pointi 15 wakati huo huo awe amefunga mabao zaidi ya matano ili amshushe kwani imefunga jumla ya mabao 12 huku Yanga ikifunga 18.

Wakati huo huo Azam Fc kama ikipata ushindi wenye mabao zaidi ya mawili basi itapanda hadi nafasi ya pili na kuishusha Simba ambayo ina pointi 15 huku ikifunga mabao 14 katika mechi tano ilizo-cheza.

Upande wa Yanga kama ikishinda katika mchezo huo basi itaendelea kuongeza gepu la pointi kwani itakuwa na 18 na kuzidi kuendelea kukaa kileleni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: