Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga, Azam FC hazina tofauti

Yanga Bingwaaaaa Yanga, Azam FC hazina tofauti

Wed, 9 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mechi ya kwanza ya Ngao ya Jamii kufungua msimu mpya wa 2023|24 itachezwa Yanga ya Gamondi vs Azam FC ya Dabo.

Ni mechi nzuri ambayo ina vitu vingi kuanzia namna ambavyo Azam imejiandaa kwa ajili ya msimu huu lakini pia maingizo mapya kutoka Yanga [Feitoto na Bangala] yanaongeza mvuto wa mechi.

Watu wanataka kuona Feitoto na Bangala ni kitu gani wanaweza kuchangia kwenye kikosi cha Azam, hilo ndio linaifanya mechi hii kuwa mechi kubwa kuliko mechi zingine ambazo zitachezwa labda wakutane Simba na Yanga kwenye Fainali.

Ukiangalia Azam na Yanga hazina tofauti kwa sababu vikosi vyao vya kwanza 70% ya wachezaji waliokuwepo wameendelea kubaki. Wamefasajili baadhi ya wachezaji kujazia nafasi zilizoachwa wazi.

Kwa hiyo unaziona timu ambazo zilishindana msimu uliopita zikiendelea kushindana msimu huu huku kukiwa na maingizo mapya ikiwa ni waalimu na baadhi ya wachezaji.

Ni mechi ya kwanza kutambulisha Azam na Yanga zipo wapi kwa sasa kuelekea kwenye msimu mpya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live