Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga, Al Hilal ngoma nzito kwa Mkapa, Vita yahamia Sudan

Khali Auchooo FT' Yanga 1-1 Al Hilal

Sat, 8 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dakika 90 za mchezo wa kwanza kati ya miwili baina ya Yanga na Al Hilal ya kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, zimekamilika kwa sare ya goli 1-1.

Yanga ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao la uongozi dakika ya 50 kupitia kwa Fiston Mayele akipokea pasi safi kutoka kwa Khalid Aucho.

Bao hilo liliwafanya Yanga kufunguka na kutaka kupata mabao mengi zaidi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele.

Mabadiliko matatu kwa pamoja waliyoyafanya Hilal yalileta tija baada ya Abdelrahman Yusuf kuipatia bao Al Hilal la kusawazisha.

Sare hii inafanya mchezo wa mkondo wa pili kuwa mgumu zaidi utakaopigwa nchini Sudan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live