Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Al Ahly wamekuja wakati mbaya, tunapiga!

Ally Kamwe Awajibu Mashabiki Young Africans.png Yanga: Al Ahly wamekuja wakati mbaya, tunapiga!

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga SC wamesema wapinzani wao katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly wamekuja wakati mbaya hivyo lazima waziache alama tatu kwa Mkapa jijini Dar.

Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema Al Ahly amekuja wakati ambao wao wametoka kupoteza goli 3-0 dhidi ya CR Belouizdad na wana mpango wa kuvuna alama zote tatu za nyumbani.

"Wwamekuja wakati mbaya na sisi tunazitaka alama tatu za nyumbani, wamekuja tukiwa tunahitaji ushindi wa nyumbani kurudisha heshima yetu baada ya kupoteza," alisema Kamwe.

Yanga watakuwa na kibarua cha kuwavaa Al Ahly ambao wanaongoza kundi lao wakiwa na alama 3 huku Yanga wakiwa na sifuri sambamba na Medeama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live