Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga, Al Ahly hesabu kali, rekodi zaibeba Kwa Mkapa

Al Ahly Yanga Ms Yanga, Al Ahly hesabu kali, rekodi zaibeba Kwa Mkapa

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hesabu kali kwa Yanga ni kuhakikisha inaibuka na ushindi kwenye mchezo ujao dhidi ya Al Ahly ya Misri kwenye Uwanja wa Mkapa Jumamosi.

Yanga itakuwa mwenyeji wa bingwa huyo mtetezi, kwenye mchezo wa pili wa makundi ambapo kwa namna yoyote wanapaswa kushinda kufufua matumaini baada ya kupoteza ugenini kwa bao 3-0 dhidi ya CR Belouzdad ya Algeria, huku Ahly ikiibuka na ushindi kama huo dhidi ya Medeama ya Ghana.

Yanga imekuwa na kikosi bora kwenye michuano yote kwa msimu wa pili sasa, msimu uliopita ilifanikiwa kufika hatua ya fainali ya Shirikisho Afrika ikiwa imevuka vigingi vikubwa. Ubora wa Yanga upo kwenye maeneo mengi, lakini kasi yao uwanjani, ubora wa safu ya ulinzi na aina ya kumiliki mpira ni mambo ambayo lazima yaipe hofu kubwa Ahly ambao mara ya mwisho ilitua hapa nchini mwezi uliopita na kutoka sare ya mabao 2-2 na Simba.

Pamoja na Yanga kulala kwa mabao 3-0 dhidi ya Belouzdad lakini ilionekana kuonyesha ubora wa hali ya juu, jambo ambalo linaweza kuwapa ushindi kwenye Uwanja wa Mkapa Jumamosi.

YANGA BORA KWA MKAPA:

Msimu uliopita ukiachana na mechi ya USM Algier, Yanga haijawahi kupoteza mchezo wowote kwa Mkapa, ikiwa ilifanya vizuri kwenye mechi zote za shirikisho la hadi sasa haijapoteza mchezo wowote kwenye uwanja huo, uwe wa ligi au kimataifa msimu huu.

AHLY ILICHEZEA:

Mara ya mwisho Ahly ilipoteza bao 1-0 dhidi ya Yanga hapohapo Benjamin Mkapa. Bao la kichwa la aliyekuwa nahodha, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kwenye mchezo ambao walionekana kuwa wanaweza kuibuka na ushindi wa mabao mengi zaidi, jambo ambalo linaonekana kuwa ni rahisi kwa mabingwa hao wa Tanzania kurudia historia hiyo. Katika michezo 10 ya jumla ambayo wamekutana Ahly wameshinda 6, Yanga moja na sare tatu.

MIFUMO WANAYOTUMIA

Mifumo mikubwa miwili ya Ahly wanayotumia ni 4-3-3 na ule ambao sawa na Yanga wanaoutumia wa 4-2-3-1 wakitegemea wanakutana na timu ipi.

Ilipokuja nchini mwezi uliopita kucheza dhidi ya Simba kwenye ufunguzi wa African Football League walitumia mfumo wa 4-2-3-1 ambao pia ulitumia na Wekundu hao wa Msimbazi tena kwenye mechi zote mbili, endapo Ahly akitumia mfumo huo kwa Yanga itakuwa ngumu kwao kushinda kutokana na wachezaji wengi wa Yanga kuwa na kasi zaidi wanapocheza kuliko Ahly.

Ahly wakiwa ugenini huwa hawatangulizi sana kushinda, hucheza kwa asilimia 60 pekee ikitegemea na ubora wa mpinzani huku wakitumia silaha la kujiangusha,kulalamika na kupoteza muda ili kupata sare jambo ambalo linaweza kuwasaidia Yanga ambao kwenye nafasi tatu ambazo wamekuwa wakipata mbili wamezitumia vizuri.

MASTAA HATARI

Ahly mara nyingi huwatumia watu watano hatari ugenini ambao ni Reda Slim, Emam Ashour, Percy Tau, Salah Mohsen ambaye mara kwa mara amekuwa akipishanishwa na Mahmoud Kahraba ambao mmoja wao huwa mshambuliaji wa mwisho, hata hivyo Yanga wanaweza kupambana nao kwa kuwa wana safu bora ya ulinzi pamoja na kiungo.

Pamoja na kuruhusu mabao matatu ugenini, lakini Yanga wamekuwa bora kwenye ulinzi wakiwa wanawatumia zaidi, Dickson Job, Bakar Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Joyce Lomalisa na Yao Kouassi huku eneo la kiungo wakiwategemea zaidi Aziz Ki, Pacome Zouzou na Maxi Nzengeli ambao wamekuwa bora kwenye michezo mingi.

BEKI YAO Yanga inatakiwa kuwalazimisha Ahly kufanya makosa ili watumie makosa ya safu yao ya ulinzi ambayo inaruhusu mabao kama wakipata presha.

Kwenye mechi zao tatu za kimataifa Afrika msimu huu Ahly imeruhusu mabao manne ambapo matatu kati ya hayo imeyaruhusu dhidi ya Simba.

Mchezo wa mwisho Ahly kupoteza ni ule wa ugenini dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ukiwa ni mchezo wa marudiano wa African Football League ambao uliwatupa nje ya mashindano hayo.

UDHAIFU AHLY

Ahly inawatumia mabeki wa pembeni kupandisha mashambulizi yao ambao ni Mohamed Hany lakini mtu hatari zaidi ni Ali Maaloul ambaye anacheza beki ya kushoto.

Maaloul ni mjuzi wa kupiga krosi kali lakini pia ndiye mpigaji wa mipira ya adhabu ndogo na hata mpigaji wa kwanza wa penalti wa timu hiyo ambao hawa wote wawili Yanga lakini adhari zao ni kwamba wamekuwa wakipanda zaidi na kuacha mwanya ambao kama Yanga wakiutumia vizuri watapata mabao kupitian kwao.

KATIKATI NDUGU WA DIARRA Kama kuna mtu ambaye safu ya kiungo ya Yanga haitakiwi kumuacha huru kando basi ni Allou Dieng raia wa Mali ambaye anacheza timu moja ya taifa na kipa wa mabingwa hao wa Tanzania Djigui Diarra.

Dieng anajua kubadilika kusaidia ukabaji na hata kupandisha mashambulizi viungo wa Yanga Mudathir Yahaya na hata Khalid Aucho watatakiwa kufanya kazi kubwa eneo hilo.

PLUIJM NA WACHAMBUZI

Kocha mkuu wa zamani wa Yanga Mholanzi, Hans van der Pluijm alisema ili kikosi hicho kipate matokeo mazuri ni lazima kicheze kwa tahadhari na kwa nidhamu kubwa kuanzia eneo la kujilinda hadi katika ushambuliaji.

“Yanga inacheza na timu nzuri Afrika lakini haipaswi kuwaogopa kwa sababu iko nyumbani na inahitaji pointi tatu baada ya mechi ya kwanza kupoteza, naamini inaweza kushinda endapo tu itazuia vizuri na kila nafasi itakayopata itaitumia vyema.”

Pluijm ambaye ndiye kocha aliyeipa ushindi pekee Yanga mbele ya Ahly aliongeza inapaswa kutowapa nafasi wapinzani wao ya kuwashambulia kwa kuhakikisha inacheza kwa muunganiko mzuri kwani ina washambuliaji bora hivyo njia nzuri ya kuwazuia ni kucheza na kutowapa mianya ya kuwashambulia zaidi. Nyota wa zamani wa Yanga, Said Maulid ‘SMG’ alisema bado ina nafasi ya kupata matokeo chanya huku akiweka wazi kuwa; “Ukiangalia mchezo uliopita na CR Belouizdad ugenini ilicheza vizuri sana licha tu ya wao kupoteza, Al Ahly ni timu bora na yenye wachezaji wasumbufu hivyo Yanga inapaswa kucheza kwa nidhamu kubwa huku ikitambua ushindi ndio silaha yao.” Lakini Kocha Msaidizi wa Biashara United, Edna Lema alisema kundi bado liko wazi hivyo inapaswa kusahau yaliyopita na iweke nguvu za kutosha

Chanzo: www.tanzaniaweb.live