Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanayotokea Simba, Namungo sababu ni hii tu

Simba Den Pic Data Yanayotokea Simba, Namungo sababu ni hii tu

Sun, 11 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KATIKA mchezo wa soka kwa kila nchi Ligi Kuu huwa ndio mashindano ya juu kabisa ya mchezo kwa nchi, huku yakifuatiwa na mashindano ya Kombe la Shirikisho la soka la nchi hiyo ambayo kwa hapa kwetu Tanzania mashindano yanayotambulika kama Kombe la Azam Sports.

Ndio maana kutokana na ukubwa wa mashindano hayo huchangia mabingwa wa mashindano hayo kushiriki katika mashindano makubwa kabisa katika Bara la Afrika ambayo ni Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Kombe la Shirikisho ambayo kwa Bongo - klabu za Simba na Namungo ndizo zinashiriki katika mashindano hayo.

Hivyo ni ukweli usiopingika kuwa taswira ya soka la nchi husika hubebwa na mashindano hayo mawili makubwa kabisa ambayo ukubwa wake sote tunauelewa.

Kutokana na kuona kwa miaka mingi klabu zetu zinavyotwaa ubingwa wa mashindano ya ndani na kwenda kushiriki katika mashindano ya kimataifa tunakoambulia patupu, walau mwaka huu Simba na Namungo zimetutoa kimasomaso.

Tumekuwa tukiona klabu zetu zikishindwa kufanya vizuri na kutolewa katika mashindano ya kimataifa mapema hatua za awali, hivyo kubeba taswira ya soka la nchi kuwa ni la kiwango cha chini.

Related Faida za Chama, Miquissone kutamba Afrika SHAURI LA MWAKALEBELA PICHA PANAHivyo kwa msimu huu wa mwaka 2020/2021 ambapo tumeona klabu za Simba na Namungo ambazo ndizo zinazotuwakilisha katika mashindano ya kimataifa zikifanya vizuri na kuifanya timu ya Namungo FC kufanikiwa kufika katika hatua ya makundi huku timu ya Simba ikiingia kibabe katika hatua ya robo fainali.

Mafanikio hayo yamebeba taswira ya soka nje ya nchi kama nilivyosema hapo awali kuwa ushiriki wao unatokana mafanikio waliyoyapata katika mashindano makubwa kwa nchi ambayo ni Ligi Kuu pamoja na Kombe la Shirikisho la Azam Sports.

Mafanikio kama hayo ndio ambayo huwa yanatakiwa kuwa na mwendelezo ili kusaidia ukuaji wa soka la nchi, kwani leo hii tunavyoona mataifa ya Afrika kama vile Algeria, Tunisia, Morocco na Misri kila siku yamekuwa na mwendelezo wa ukuaji wa soka kwa sababu klabu kutoka katika mataifa hayo huwa zinajikita katika kufanya vizuri kimataifa kuliko kufanya vizuri katika mashindano ya ndani.

Ndio maana hata usajili wa wachezaji ambao husajiliwa huzingatia mashindano ya kimataifa hivyo kujikuta zikiendelea kufanikiwa.

Hivyo ushiriki wa klabu za soka zenye mafanikio katika mashindano ya kimataifa unatakiwa kuwa na tija kwa maendeleo ya soka la ndani iwapo tu utakuwa na mikakati ya muda mrefu kama ambavyo wenzetu wamekuwa wakifanikiwa na kujikuta ligi zao na mashindano ya makombe ya shirikisho yakiendelea kuimarika kila siku kutokana na klabu kujikita katika ushiriki wa mechi za kimataifa.

Na maandalizi haya kwa klabu ni kama vile kwa mwanafunzi ambaye anajiandaa kufanya mtihani wa kidato cha sita, hivyo akifanikiwa kuwa na maandalizi mazuri ya kufanya mtihani wa kidato cha sita, ule wa mtihani wa kidato cha nne hauwezi kumsumbua. Hii iko sawa na pale timu inapojiandaa kwa ajili ya mashindano ya kimataifa, kwa ligi za ndani haziwezi kuwasumbua sana na hivyo kujikuta kila mwaka timu zinakuwa bora zinaposhiriki katika mashindano ya kimataifa.

Mipango hiyo huanzia katika usajili wa wachezaji, kwa mfano ukiwaangalia Simba unaona kabisa kuwa wachezaji wote waliowasajili msimu huu na kipindi cha dirisha dogo wameonekana kukidhi viwango vya ushindani wa mechi za kimataifa.

Ndio maana kina Taddeo Lwanga na Rally Balya wamefika tu Simba na kuingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza, hivyo kusaidia timu kufika hapo ilipo.

Ukiangalia timu ya Namungo FC kwa hatua waliyofikia utaona kuwa ni hatua kubwa kiasi cha kuwa zaidi ya mafanikio waliyojipanga nayo kwani pamoja na kufika walipo katika Kombe la Shirikisho, lakini mpango wao wa usajili wa wachezaji wakati msimu huu unaanza ulijikita katika ushindani wa mechi za ndani huku wakiwa na wachezaji ambao wengi wao ndio wanaelekea kuwa wakubwa kama vile kina Carlos Protas, Manyanya, Lusajo na wengineo.

Ndio maana hata baada ya kucheza mechi tatu za hatua ya makundi na kupoteza zote huku Namungo ikiwa haijafanikiwa kufunga bao hata moja, haitakiwi kulaumiwa kutokana na maandalizi waliyofanya, hayakuwa na mpango wa muda mrefu hivyo kuwa ni somo la kujifunza ili timu zote zenye mipango ya kushiriki katika michuno ya kimataifa ziwe na mipango kwa kuangalia ushindani wa mechi za kimataifa na sio za ndani tu.

Hivyo timu zote zinazoshiriki katika mashindano haya mawili ya soka nchini zinatakiwa kuwa tayari kujiandaa kushindana katika mashindano ya kimataifa, sio tu kwa kusajili wachezaji, bali hata kwa kucheza mechi za kirafiki za kimataifa ili zinapopata nafasi ziweze kuitumia na kujenga taswira bora ya ligi yetu nje ya nchi.

Imeandikwa na ALI MAYAY

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz