Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yaliyowakumba Namungo yanatukumbusha uzalendo

Namungo Pic 1 Data Yaliyowakumba Namungo yanatukumbusha uzalendo

Fri, 19 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Khatimu NahekaMore by this Author WIKI iliyopita kuna vitendo vya kikatili michezoni viliikumba Klabu ya Namungo katika safari ugenini wakiwafuata wenyeji wao 1º de Agosto huko Angola katika mchezo wa kwanza wa mtoano wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Kwa mujibu wa matukio ambayo yaliripotiwa tangu kufika kwa timu hiyo nchini humo unaweza kupata picha jinsi gani bado kuna mataifa hayajajua kushindana kwa mbinu za uwanjani na kuwa na vita nje ya uwanja kuwaondolea utulivu timu wenyeji kabla ya mchezo.

Uwepo wa mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19 na taratibu zake za vipimo bahati mbaya bado Shirikisho la Soka Afrika (Caf) halijajua jinsi gani baadhi ya klabu zinavyotaka kutumia kama fursa ya kuziumiza timu zingine kabla ya kukutana uwanjani.

Hili pia lilikuwa linakwenda kuikumba Namungo nchini Angola inaonyesha wazi wenyeji wao kuna mpango maalumu waliupanga kwa wageni wao ili kuhakikisha wanavuna kabla kukutana uwanjani au wasikutane kabisa.

Kitendo cha kupimwa wachezaji wote kama wana maambukizi na kuwabaini watatu kisha kung’ang’ania timu nzima ikae karantini ulikuwa ni ukatili uliopitiliza kwa wawakilishi hawa na bahati mbaya inawatokea Namungo ambayo ni klabu changa inayoshiriki kwa mara ya kwanza mashindano.

Kwa matukio ya namna ile endapo yangekuwa yameikumba klabu kutoka Kaskazini mwa Afrika inawezekana tungeshasikia taarifa nzito ya waliofanya vitendo vile hata kupewa adhabu kali, lakini bado taarifa mpya inasubiriwa ya kipi kitaamuliwa.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz