Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yaliyomkuta Bruno Gomes Singida FG mmmh!

Bruno Barroso Tanga Yaliyomkuta Bruno Gomes Singida FG mmmh!

Sun, 24 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Singida Fountain Gate Mbrazili, Ricardo Ferreira amesema nyota wa kikosi hicho, Bruno Gomes ni suala la kisaikolojia tu linalomsumbua ingawaje bado ana matumaini makubwa atarudi katika ubora ambao mashabiki wameuzoea.

Ferreira alisema haamini kama nyota huyo ameshuka kiwango isipokuwa ni upepo mbaya tu anaokutana nao.

“Ni kweli ukiangalia takwimu zake za msimu uliopita na sasa ni tofauti kabisa kitu ambacho hata yeye kinamsumbua sana kichwani, naamini akifunga tu atarudi katika hali yake ya kawaida kwani bado kwangu ni mchezaji mzuri,” alisema.

Ferreira aliongeza jambo linalomsumbua Bruno ni saikolojia na anazidi kumjenga ili kurudi katika ubora wake huku akiweka wa-zi ujio wa nyota mwenzake, Marouf Tchakei aliyetokea AS Vita Club haujaathiri kiwango chake kama inavyosemwa na wengi.

Kwa upande wa Bruno alikiri kupitia changamoto ya kutofanya vizuri huku akieleza ni jambo la kawaida kwa mchezaji yeyote kwani huwezi kucheza katika kiwango kizuri kila msimu ingawa anaendelea kupambana.

Msimu uliopita nyota huyo alionyesha kiwango kizuri na kufunga jumla ya mabao 10 katika Ligi Kuu Bara na kuzivutia klabu mbalimbali za Yanga na Simba kuhitaji saini yake ila msimu huu mambo yamekuwa magumu kwake kwani hajafunga bao lolote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live