Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yajue kwa undani mashindano ya FIFA Series

FIFA QATAR Yajue kwa undani mashindano ya FIFA Series

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: Rick

Katika Mpango kazi mpya wa FIFA kuwa karibu na Wanachama wake mwaka 2022 FIFA Council ilipitisha utaratibu ambao kutakuwa na Mashindano au michezo itayohusisha Wanachama wake toka Mabara yote yatayofanyika katika vituo maalum yatayoandaliwa na FIFA wenyewe ili kuwapa Wanachama wake fursa, uwezo, uelewa zaidi, kujifunza na kutoa Nafasi kwa Nchi ambazo ni ngumu kupata nafasi kama hizo kwa kiwango kile kile wanazopata wengine katika madaraja ya juu na kuita mpango huu ni FIFA SERIES.

FIFA SERIES 2024

Ni Mashindano ambayo yameandaliwa kwa Asilimia 100 na FIFA kama Pilot Project kwa Mataifa wanachama wake (nchi) 20 Duniani kote toka Mabara yote 6 na kufanyika katika Vituo Vitano vilivyopo katika Mataifa Manne tofauti tofauti toka mabara Matatu.

Mashindano haya yatakuwa yanafanyika kila Mwaka katika muda wa FIFA CALENDAR na mwaka huu 2024 ni MARCH 18-26, na Mwaka huu yatafanyika Algeria, Saudi Arabia A na B , Sri Lanka na Azerbaijan kwa kila Kituo kuna na Timu 4.

DHUMUNI KUBWA LA FIFA Katika Project ya FIFA SERIES imekusudiwa kuwa uchanguzi wa nchi Shiriki uendane na Mazingira, Utamaduni, Uwezo na Ushawishi ili kuweza kupata vitu vyote hivi mbadala vitavyowezesha baada ya Kila Project kuwe na Mambo Chanja yenye Exposure kwa wahusika, kuanzia katika maandalizi, Safari, Camp, Malazi, Mazoezi na mpaka mechi ili kutoa fursa kwa ambao hawezi kupata hizi nafasi kwa ufahisi kuwa kweli kirahisi.

TANZANIA NA FIFA SERIES

Tanzania imepata bahati ya kuwa moja ya nchi Wanachama wa FIFA kuwepo katika mradi wa kwanza wa majaribio (Pilot Project) ya Uhusiano mwema ya FIFA SERIES katika Africa yaani CAF imetoa nchi Nne tu ambazo ni Tanzania, Algeria, South Africa na Guinea.

Mashindano haya yamepangwa muda mrefu toka 2023 na kuratibiwa Moja kwa moja na FIFA wenyewe na mpango kazi wa kila kitu ulishawekwa tayari toka January 2024 ilibaki utekelezaji tu muda huu wa Mwezi March 2024.

Tanzania itapata bahati ikiwa imepangwa Kituo cha Azerbaijan pamoja na Bulgaria, Mongolia na Azerbaijan wenyeji itacheza michezo miwili dhidi ya Mongolia na Bulgaria ambao hawa ni wakubwa.

Chanzo: Rick