Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yahya Zayd arejea baada ya wiki nane

Yahya Zaid Mkataba Yahya Zayd arejea baada ya wiki nane

Fri, 13 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiraka wa Azam FC, Yahya Zayd amerudi mdogo mdogo baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki nane akiuguza majeraha ya goti.

Akizungumza na Mwanaspoti, Daktari wa Azam FC, Mbaruku Mlinga alisema baada ya kukamilisha matibabu yake amemkabidhi kwa kocha wa viungo ili kumwangalia na kumjenga kimwili kabla ya kujiunga na wenzake chini ya kocha mpya wa timu.

“Hawezi kujiunga moja kwa moja na timu lazima apite chini ya kocha wa viungo ili kurudisha mwioli kwenye utimamu kwa kuanza mazoezi mepesi hicho ndio kinafanyika kwa sasa lakini kwa asilimia 100 amerudi kwenye utimamu,” alisema Dk Mlinga na kuongeza;

“Akiwa na kocha wa viungo anafanya mazoezi mepesi kama kukimbia, kufanya mazoezi ya viungo bila mpira na baadae na mpira baada ya hapo ndio anajiunga pamoja na timu tayari kwaajili ya kumshawishi kocha kama anaweza kumtumia kwa mechi ya ushindani kwa dakika chache na baadae kucheza kwa dakika ote 90 kulingana na utimamu wake.”

Mlinga alisema hakuna uwezekano wa kiraka huyo kuuwahi mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa leo dhidi ya Pamba kwani ndiyo kwanza karejea jana na kukabidhiwa chini ya kocha wa viungo ambaye atamtazamia kwa muda kabla ya kumruhusu kujiunga na wenzake.

Nyota huyo aliyedumu kikosini hapo kwa muda mara baada ya kurejea kutoka Misri amekuwa panga pangua kikosi cha kwanza na kuonyesha ubora eneo la kiungo mkabaji akiongeza nguvu eneo la ulinzi linaloongozwa na Yeison Fuentes.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live