Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yahya Njenge: Kocha analazimisha wachezaji wake wapya wacheze

Dabo Azam 128.png Makocha wa Azam FC

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Azam FC Youssouph Dabo bado mgeni kwenye timu na Ligi pia, lakini naamini kadiri siku zinavyozidi kwenda anazidi kuijua timu yake na kupata suluhisho la changamoto anazokutana nazo kadiri anavyopanga kikosi chake.

Sioni kama Dabo anaisoma vizuri timu yake na kufanya maamuzi sahihi hususan katika upangaji wa kikosi chake. Namna anavyopanga kikosi chake sidhani kama anaisaidia Azam!

Kikosi alichokipanga dhidi ya Dodoma Jiji tayari nilianza kuhisi kutakuwa na changamoto kwa Azam FC kupata goli. Kwenye eneo la ushambuliaji kulikuwa na Mbombo, Diao na Sida.

Timu ina Idd Nado, Sopu, Lyanga na Kipre Jr hawa wote ni washambuliaji bora wenye uwezo wa kucheza wakitokea pembeni lakini owte kwa pamoja wanaanzia nje!

Kocha ni kama analazimisha baadhi ya wachezaji ambao wamekuja katika wakati wake lazima wacheze hata kama hawajainesha viwango vya kuridhisha na kuisaidia timu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: