Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yacouba wa Yanga anarudi

Yacouba Songne Mks Yacouba wa Yanga anarudi

Fri, 1 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unamkumbuka Yacouba Songne aliyewahi kukiwasha akiwa Jangwani na kikosi cha Yanga akimaliza kama kinra wa mabao wa klau hiyo msimu wa 2020-2021 akifunga manane, kisha akaumia na kukaa nje kwa mwaka mzima kabla ya kuibukia Ihefu msimu uliopita?

Kama hujui, jamaa alikuwa Arta Solar 7 ya Djibouti akikiwasha baada ya kuvutiwa na dau nono akiitema Ihefu, sasa mshambuliaji huyo wa zamani wa Asante Kotoko ya Ghana ameshtukia jambo kule aliko na fasta ameweka wazi anarudi tena nchini kucheza, kwani kuna utofauti mkubwa wa ligi ya Bongo na Djibouti.

Akizungumza nasi kutoka Djibouti, Yacouba alisema licha ya kupata fedha za kutosha akiwa huko, lakini amegundua ligi ya nchini humo bado haina ushindani mkubwa kulinganisha na ile ya Tanzania aliyoiacha.

Yacouba alisema ameanza hesabu upya za kurejea nchini kucheza, akivizia dirisha dogo litakalofunguliwa katikati ya mwezi huu na kufungwa Januari 15 mwakani, ili aje kuendeleza ule moto kwa lengo la kulinda kipaji chake badala ya kuendelea kucheza ligi nyepesi huku akivuna fedha za kutosha.

Msimu uliopita aliposajiliwa na Ihefu kwenye dirisha dogo mshambuliaji huyo raia wa Burkina Faso alifungia mabao matatu kabla ya Arta Solar kuvutiwa naye na kumpa mkataba baada ya kuomba kutoongeza mkataba mpya kwa Wana Mbogo Maji walinusurika kushuka daraja.

“Ligi ya huku sio ngumu kabisa, nakubaliana kwamba malipo yao ni tofauti na Tanzania kwa kile nilichokuwa nalipwa, lakini hapa unaweza kufifisha kipaji, hawa hawachezi soka la ushindani mkubwa,” alisema Yacouba na kuongeza;

“Ni bora nirudi Tanzania ambako ligi ya huko hata kama malipo yao sio makubwa kama huku, lakini unaona unacheza mashindano ambayo yana ushindani mkubwa na yanakujenga zaidi kuliko kucheza huku.

Aidha Yacouba alithibitisha tayari amekuwa na ofa mbili za klabu hapa Tanzania zilizokuwa zikiwasiliana naye ambapo atafikiria kurudi nchini kuanzia dirisha dogo la usajili.

“Kuna klabu kama mbili zinanihitaji hapo Tanzania, tangu nilipokuja hapo kwenye mechi za CAF ikiwa na Arta Solar, nilikuwa nawasiliana nao na waliniambia kama nitafikiria kuondoka basi niwajulishe haraka.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live