Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yacouba swahiba wa Mayele aipigia 'salute' Bongo

Yacouba Sidi Ethmane Yacouba swahiba wa Mayele aipigia 'salute' Bongo

Wed, 3 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa klabu ya Alkhoums kutoka nchini Libya, Yacoub Sidi Ethmane amesifu hatua kubwa iliyopigwa na klabu za Tanzania.

Yacoub Sidi raia wa Mauritania amesema ndani ya miaka miwili Ligi Kuu ya NBC imekuwa miongoni mwa timu bora Afrika na hilo limechangia kuwa na klabu zenye ubora pia.

Ligi ya Tanzania ni ligi bora, na katika kipindi cha miaka miwili iliyopita imekuwa moja ya ligi kali za Afrika na kuna maendeleo ya wazi kwa timu za Tanzania,” amesema Sidi.

Akipiga stori nasi kiungo huyo amesema aliwahi kucheza pamoja na Fiston Mayele, Jesus Moloko na Juma Wadol Shibani wakiwa As Vital ya DR Congo.

Amesema kwake isingekuwa tu heshima kucheza Tanzania kwani rafiki zake hao kucheza Yanga pia ni heshima kwake.

Kinachomvutia Sidi katika ligi Ya Tanzania ni uaminifu wake wa ajabu kwa wapenda soka . Amesema kwa sasa anatamani kucheza Ligi ya Misri.

“Kila mchezaji alikuwa na ndoto ya kucheza soka katika umri mdogo, na namshukuru Mungu, ndoto yangu ilitimia na nikawa mchezaji wa kimataifa,” ameongeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live