Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yacouba hana hiyana na Moloko

Yanga22 Mshambuliaji wa Yanga, Yacouba Sogne

Mon, 1 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji raia wa Burkina Faso, Yacaouba Sogne ndiye anayemng’arisha winga Mkongomani Jesus Moloko. Moloko ni kati ya wachezaji wapya waliosajiliwa na timu hiyo katika kuiimarisha safu ya ushambuliaji ya Yanga.

Winga huyo amesajiliwa Yanga kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Mkongomani, Tuisila Kisinda aliyeuzwa Berkane ya Morocco.

Yacouba akicheza michezo minne ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar, KMC FC, Geita Gold na Azam FC amehusika katika mabao mawili ambayo amefunga Moloko kwa kumpigia asisti nyota huyo.

Mabao hayo amehusika Moloko katika mchezo dhidi ya Geita Gold na Azam uliochezwa juzi Jumamosi katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

Yacouba alianza msimu kwa spidi ndogo kwa kuanzia benchi katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao alitokea benchi kuchukua nafasi ya Farid Mussa.

Mburkinabe huyo hivi sasa amejihakikishia nafasi kubwa ya kuanza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo inayofundishwa na Nasreddine Nabi. Kiungo mchezeshaji Feisal Salum ‘Fei Toto’ naye amepiga asisti mbili katika timu hiyo akicheza michezo minne ya ligi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live