Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yacouba atikisa Ihefu

Yacouba Songne Ihefu Winning Mshambuliaji wa Ihefu, Yacouba Songne

Tue, 28 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ihefu inaendelea kutesa Ligi Kuu Bara huku moto wa kiungo mshambuliaji, Yacouba Sogne ukiendelea kuwaka na kumfanya kocha mkuu wa timu hiyo, John Simkomo kuchekelea akisema yeyote wanayekutana naye lazima achezee kipigo.

Timu hiyo ambayo haikuwa na mwanzo mzuri kwa sasa imeonekana kutakata baada ya kuvuna pointi saba kwenye mechi tatu mfululizo na kukaa nafasi ya saba kwa pointi 30.

Ihefu iliyoanza kunolewa na Zuberi Katwila kisha kuongezewa nguvu kumleta Juma Mwambusi ambaye walishindwana na kutimka, kwa sasa iko chini ya mkongwe, Mkoko aliyeingoza mechi mbili sasa.

Hata hivyo, katika mechi saba ilizocheza, Ihefu imepoteza mchezo mmoja dhidi ya Yanga, sare moja mbele ya Singida BS na kushinda mitano na kujiweka sehemu nzuri kabla ya kumaliza msimu.

Yacouba ambaye alisajiliwa dirisha dogo ameendelea kuwatesa makipa kwani katika mechi mbili alizocheza amefunga mabao mawili akianza na Singida BS kisha juzi akawanyoosha Dodoma Jiji wakati chama lake likishinda 2-1 ugenini.

Mkoko alisema matokeo hayo ni mkakati wa timu kuhakikisha kila mchezo wanapata pointi tatu ili kumaliza ligi nafasi nzuri akipiga mkwara kuwa yeyote anayeingia anga zao lazima achezee kipigo.

Kocha huyo mkongwe hakusita kuwapongeza nyota wake kwa soka wanaloonesha lenye ushindani akibainisha kuwa kwa sasa wanafidia kile walichopoteza huko nyuma bila kujali wanacheza na nani na wapi.

“Kimsingi ni kuendelea kupambana ligi haijaisha na Ihefu bado ina uhitaji wa pointi hivyo lazima tujipange kila tunayekutana naye tunachukua alama tatu ili kufikia malengo,” alisema Mkoko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live