Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yacouba amuwashia taa ya njano Tuisila Kisinda

Yqcouba Yqnga Nm.jpeg Yacouba amuwashia taa ya njano Tuisila Kisinda

Sun, 30 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tangu arudi Yanga winga Tuisila Kisinda hajawa na kiwango bora, lakini nyuma ya pazia Yacouba Sogne ameendelea kupiga tizi na kama atakuwa fiti huenda akarejeshwa kikosini dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa Desemba.

Iko hivi. Kisinda yupo Yanga kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea RS Berkane ya Morocco na ametimiza idadi ya wachezaji 12 wa kigeni kikosini, lakini mabosi wa chama hilo wanaangalia mwenendo wake na kama hatarudi kwenye ubora aliounyesha misimu miwili nyuma kabla ya kuondoka Yanga huenda wakaachana naye.

Wakati huohuo, Yacouba aliyepata majeraha makubwa msimu uliopita ameendelea kufanya mazoezi maalumu kambini na Yanga licha ya kwamba hayupo kwenye usajili wa sasa na Mwanaspoti linajua kama atakuwa fiti kufika dirisha dogo atarudishwa kundini kuchukua nafasi ya mmoja wa wachezaji wa kigeni akiwemo Kisinda.

Chanzo cha ndani kutoka Yanga kimeeleza kuna mipango ya kufanya usajili wa wachezaji wasiopungua watatu kwenye dirisha dogo msimu huu akiwemo beki wa kati akitajwa kuwa kitasa cha maana na washambuliaji ambapo hilo litailazimu kupungaza mastaa wa kigeni waliopo kwa sasa na majina ya Kisinda, Heritier Makambo na Jesus Moloko yapo kwenye listi hiyo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Yacouba ameeleza kuendelea kujinoa ili arejee kwenye makali yake na kuweka wazi mipango yake.

“Jeraha nililolipata lilinifanya nikae nje kwa muda mrefu, hivyo nalazimika nifanye sana mazoezi ili kuwa fiti.

“Kwa sasa nimepona na naendelea na programu maalumu ili kurejea kwenye ubora wangu na siku sio nyingi mtaniona uwanjani,” alisema Yacouba anayesifika kwa kasi, chenga na kupachika mabao akitokea pembeni na hata mshambuliaji wa kati.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live