Sat, 13 Nov 2021
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Kiungo mshambuliaji wa Yanga Yacouba Songne ambae amepelekwa nchini Tunisia kwa ajili ya matibabu ya majeraha yake ya goti, amefanyiwa upasuaji wa goti.
Katika taarifa iliyotolewa na klabu ya Yanga imesema upasuaji huo umeenda vyema na mchezaji anatarajiwa kukaa nje kwa muda mfupi akiuguza majeraha.
Yacouba alipata majeraha katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting na kufanyiwa mabadiliko.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live