Baada ya kukaa nje kwa muda kutokana na kusumbuliwa na goti, mshambuliaji Yacouba Songne ameanza mazoezi mepesi.
Songne amefanyiwa upasiaji wa goti na aliloumia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting mchezo uliochezwa uwanja wa Mkapa.
Mshambuliaji huyo aliyekuwa anatembelea magongo ameruhusiwa kuachana nayo na sasa anatembea kawaida.
Kwa mujibu wa Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh alisema aliacha kutumia magongo siku walipocheza mchezo wa Kombe la Azam (ASFC) na mazoezi mepesi kaanza leo (Ijumaa).
“Atakuwa chini ya uangalizi wa daktari kwaajili ya kuhakikisha anaendana na ratiba ya daktari,” alisema.