Wakati anapata jeraha kubwa la goti (ACL) na kukaa nje kwa miezi 9, wengi walitafasiri ni mwisho wa Yacouba. Si hivyo tu, ikatokea anaachwa na Yanga ndio kabisa ikawa noma ghafla akaibukia Djibouti huko akitafuta ugali.. ndio ikaonekana ameuzika mpira wake.
Yacouba ni yule mwanaharakati uwanjani, muda wote anawaza kwenda mbele.. lakini akifika langoni, anapatwa na kiwewe.
Akiwa Yanga, Yacouba ndiye mchezaji aliyekuwa machachari na hatari muda wote.. na hata Nabi alipoijenga timu, bado Yacouba ndiye alikuwa anajikuta kwenye nafasi nzuri ya kufunga kuliko wengine.
Ukimcheki kule Tabora United. Yaxouba hajabadilika. Baeo ni mtu hatari na machachari uwanjani muda wote yeye anataka kukimbizana na watu.. siku zote kumkaba Yacouba, ni zaidi ya vurugu.. maana muda wote atakusumbua.
Mpira ni kama baiskeli tu. Ukiujua, ukiwa na kipaji.. umeujua.. ndio anachotupatia Yacouba Songne.