Mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Dodoma Jiji na Ihefu umemalizika jana katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma kwa wenyeji kukubali kichapo cha mabao 2-1.
Mabao ya Ihefu yamefungwa na Nelson Okwa na Yacouba Sogne huku lile la Dodoma Jiji likifungwa na Muhsin Makame.
Okwa na Yacouba wamesajiliwa katika dirisha dogo la usajili wakitokea timu za Yanga na Simba.
Zifuatazo ni dondoo muhimu za mchezo huu
Huu unakuwa mchezo wa 14 kwa Dodoma Jiji kupoteza ikishika nafasi ya pili kwa kupoteza michezo mingi,vinara wakiwa Ruvu Shooting waliopoteza michezo 15.
Bao la Okwa ni la kwanza kwake tangu ajiunge na klabu hiyo katika dirisha dogo la usajili akitokea Simba.
Bao la Yacouba Songne ni la pili kwake tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Yanga,bao lake la kwanza lilikuwa dhidi ya Singida Big Stars.
Muhsin Malima hilo linakuwa bao lake la pili msimu huu,la kwanza alilifunga dhidi ya Azam katika mchezo uliomalizika kwa Dodoma Jiji kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Ushindi wa leo unaisogeza Ihefu katika nafasi ya saba wakiwa na pointi 30 huku Dodoma Jiji wakiendelea kubaki katika nafasi ya 12 wakiwa na pointi 24.