Wakati Ihefu ikitarajia kushuka uwanjani baadaye kuwavaa Simba, kocha mkuu wa timu hiyo John Simkoko amefanya mabadiliko ya wachezaji watano kuanza mechi hiyo ikilinganishwa na kikosi kilichocheza mchezo uliopita wa kombe la shirikisho (ASFC) dhidi ya Wekundu hao Aprili 7.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa robo fainali, Ihefu ilibutuliwa mabao 5-1 na kutupwa nje kwenye michuano hiyo huku Simba ikifuzu nusu fainali ya ligi hiyo sawa na watani zao Yanga, Singida Big Stars na Azam FC.
Katika kikosi kilichocheza mechi hiyo, wachezaji kipa Fikirini Bakari, beki Nico Wadada na mshambuliaji Obrey Chirwa hawakuwapo kabisa huku Yacouba Sogne na Adam Adam walioanzia benchi wameanza leo.
Kikosi chenyewe hiki;
Fikirini Bakari
Nico Wadada
Yahya Mbegu
Juma Nyosso
Lenny Kisu
Samuel Onditi
Obrey Chirwa
Raphael Daud
Yacouba Sogne
Adam Adam
Joseph Mahundi
Wanaosubiri ni Hussein Masalanga, Mwaita Gereza, Hassan Mwasapili, Ally Ally, Said Makapu, David Mwantika, Peter Mwalyanzi, Isah Ngoah na Midathir Abdul.
Ihefu inashuka uwanjani ikikumbuka ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam kwenye uwanja wake wa Highland Estate, huku ikipoteza dhidi ya wapinzani hao mchezo wa ASFC dhidi ya Wekundu hao 5-1. Hadi sasa Simba wapo nafasi ya pili kwa pointi 57 huku Ihefu wakiwa nafasi ya sita kwa alama 30.