Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

YANGA YAAHIDI KUMLIPA TAMBWE

0ecc814e81be61f7036abe5c7d7c33cf YANGA YAAHIDI KUMLIPA TAMBWE

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MUDA mfupi baada ya kuwapo kwa taarifa kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kuwa imeifungia Yanga kusajili misimu mitatu kwa kushindwa kumlipa mchezaji wake wa zamani, Amis Tambwe deni la Sh milioni 41, klabu hiyo imeahidi kuweka mambo sawa.

Tambwe aliyeitumikia Yanga kwa zaidi ya misimu miwili iliyopita, amesema anaidai klabu hiyo fedha zake za usajili na mishahara. Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali jana zilieleza kuwa, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Dk Mshindo Msolla hana shida juu ya hilo na ameahidi kulipa deni hilo kama ilivyotokea kwa wengine waliokuwa wanadai huko nyuma.

“Tuna utaratibu wetu wa kulipa madeni na FIFA wana ufahamu tunalipa nusu nusu na hata George Lwandamina na Mwinyi Zahera tuliwalipa hivyo na Tambwe atalipwa kwa utaratibu huo,” alisema.

Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Hersi Said alisema ndani ya wiki hii watahakikisha wanakamilisha deni hilo. Aliwataka mashabiki na wanachama wa Yanga kutokuwa na wasiwasi kwani wapo imara kuijenga klabu hiyo ndani na nje ya uwanja kwa kuwapa kilicho bora.

Awali, Wakili wa Tambwe, Felix Majani alisema Yanga ikikamilisha deni hilo itafunguliwa kifungo hicho na kuendelea na utaratibu wa kawaida. Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Ismail Rage alihimiza klabu hiyo kuheshimu mikataba ya wachezaji wao.

Alisema Yanga wanatakiwa kulipa fedha hizo haraka iwezekanavyo na kadiri wanavyochelewa wanaweza kuingia kwenye hatari ya kuondolewa kwenye mashindano ya aina yoyote ya kimataifa na hata kuigharimu timu ya taifa kutoshiriki mashindano ya Afrika baadaye.

Chanzo: habarileo.co.tz