Kocha wa Barcelona, Xavi Hernandez amethibitisha mabosi wa timu hiyo wapo kwenye mchakato wa kuhakikisha staa wao wa zamani, Lionel Messi ambaye kwa sasa anaichezea PSG anarudi kwenye kikosihicho msimu ujao.
Messi ambaye mkataba wake na PSG umemalizika mwisho wa msimu huu, amekuwa akitajwa huenda akatimkia zake Saudi Arabia na Al Hilal inataka kumpa zaidi ya Pauni 500 milioni kwa mwaka ili kumsajili.
Barca wamekuwa wakipambana kumrudisha na taarifa zinadai kuwa tayari mazungumzo baina ya mabosi wa timu hiyo na wawakilishi wa Messi yameshaanza. Xavi pia amekuwa akitumia ukaribu wake na staa huyu kumshawishi akubali kutua kwenye kikosi chao.
Hata hivyo, ili kumsajili Barca itatakiwa kuuza baadhi ya wachezaji muhimu dirisha lijalo ili kuendana na sheria ya matumizi ya pesa La Liga.