Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Xavi atangaza kuachana na Barcelona

Barcelona Legend Xavi Hernandez 2021 Xavi atangaza kuachana na Barcelona

Sun, 28 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Xavi Hernandez amekubali yaishe baada ya kutangaza kuachana na klabu yake mwisho wa msimu huu.

Xavi ambaye ni kiungo wa zamani wa Barca ametangaza uamuzi huo leo mara baada ya timu yake kukubali kipigo kikali Cha mabao 5-3 kutoka kwa Villarreal.

Kipigo hicho kimeifanya Barca kubaki nyuma kwa alama 10 dhidi ya vinara wa Ligi Real Madrid ambao mapema leo wameendeleza moto kwa ushindi wa mabao  2-1 ugenini dhidi ya Las Palmas.

Mara baada ya kipigo hicho Cha Barca Xavi ameonekana kuwa na uso wa simanzi nzito akitafakari kabla ya kwenda kutangaza uamuzi huo mgumu.

Msimu huu Barca chini ya Xavi kwenye mechi zake 21 za Ligi imefanikiwa kushinda 13 ikipoteza 3 na kutoa sare 5, ikiwa nafasi ya tatu na alama zao 44 huku Girona wakiwa nafasi ya pili na alama zao 52.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live