Siku kadhaa baada ya Xavi Hernandez kutambulishwa rasmi kama kocha mkuu wa timu ya Barcelona, klabu imethibitisha na kutangaza benchi lake la wasaidizi.
Xavi amerudi baada ya kuachana na klabu kwa muda wa miaka sita alipoondoka kama mchezaji na Mkongwe katika korido za Camp Nou, na sasa amerudi kama kocha mkuu ambaye ana kazi kubwa ya kuirudishia heshima klabu iliyopoteza baada ya matokeo mabovu chini ya Ronald Koeman.
Benchi la Hernandez litakuwa na watu saba ambao ni, kaka yake Oscar Hernandez na Sergio Alegre watakuwa makocha wasidizi, Ivan Torres atakuwa kocha wa “fitness”, Sergio Garcia, Toni Lobo na David Prats watakuwa watu wa tathimini wakati Jose Ramon De la Fuente kocha wa makipa na mtu pekee aliyabaki kutoka kwenye benchi la Koeman.
Xavi ataanza kibarua chake kama kocha mkuu wa barcelona baada ya mapumziko ya kimataifa kuisha na mchezo wake wa kwanza utakuwa dhidi ya Espanyol kwenye dimba la Camp Nuo tarehe 20 novemba kwenye La Liga