Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Xavi atambulishwa rasmi Barcelona (+Video)

Xavi (600 X 750) Meneja Mpya wa Barca Xavi Hernandez

Mon, 8 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa zamani wa Barcelona, Xavi Hernandez ametambulishwa rasmi kuwa meneja wa kikosi hicho cha Catalunya, akishika nafasi iliyoachwa na Ronald Koeman ambaye alitimuliwa mwezi uliopita.

Akizungumza mara baada ya utambulisho huo Xavi amesema "Tuna kazi kubwa ya kufanya kila siku. Sisi ni Barcelona, klabu bora ulimwenguni, na hii ndio njia pekee ya kupata matokeo. Tunataka tucheze mpira utakaomvutia kila mtu, kama wananilinganisha mimi na Pep Guardiola, ni katika mambo mazuri. Pep ni Kocha bora ulimwengunni".

Aidha Xavi ameweka wazi dhamira yake ya kutaka kumbakisha winga wa Ufaransa Ousmane Dembele kama mkakati wake wa kwanza kwa kumshawishi asaini mkataba mpya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live