Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Xavi apata dawa ya ushindi Barca

Barca Win 4 27 Barca imeibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Athletic Bilbao

Mon, 28 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

FC Barcelona imeendelea kuwa na kiwango bora baada ya Jumapili kuishindilia Athletic Bilbao goli 4-0 huku mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang akifunga goli moja kwenye ushindi huo.

Magoli ya Barcelona ambao walikuwa nyumbani katika dimba la Camp Nou yamefungwa na Aubameyang ambaye ni bao la tano kwenye msimu huu ingawa amejiunga na Barca dirisha dogo la Februari, Ousmane Dembele ambaye alikuwa na ubora mzuri akafunga goli la pili kisha Luuk de Jong na Memphis Depay wakafunga magoli yao na kufanya matokeo kuwa 4-0.

Ni wachezaji wawili tu ambao wamefunga goli zaidi ya Aubameyang nyota wa zamani wa Arsenal, Depay (9) na De Jong (6).

Kwa matokeo hayo yanaifanya Barcelona kukaa nafasi ya nne mbele ya Mabingwa watetezi Atletico Madrid mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Hispania La Liga kwa kufikisha alama 45 kwenye nafasi nne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live