Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Xavi anatoka, Flick anaingia Barcelona

Xavi X Flick Xavi anatoka, Flick anaingia Barcelona

Mon, 27 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

NDO hivyo. Barcelona imemfuta kazi Xavi baada ya kuinoa timu hiyo kwa miaka mitatu.

Miamba hiyo ya Nou Camp imepanga kutangaza kocha mpya ndani ya siku chache zijazo.

Barca imethibitisha taarifa hiyo ya kocha Xavi kuondolewa kazini na ataondoka jumla Nou Camp baada ya mchezo wa mwisho wa La Liga, utakaopigwa leo Jumapili dhidi ya Sevilla.

Wakati huo huo, Fabrizio Romano aliripoti kwamba Hansi Flick anajiandaa kutangazwa kuwa kocha mpya wa Barcelona wiki ijayo. Mjerumani huyo amesaini mkataba wa miaka miwili na ataandamana wasaidizi wake wawili kama sehemu ya benchi la ufundi la miamba hiyo ya Nou Camp.

Kocha huyo wa zamani wa Bayern Munich, Flick amekuwa hana kazi tangu alipoachana na timu ya taifa ya Ujerumani, Septemba mwaka jana. Alikuwa akihusishwa pia na mpango wa kwenda kurithi mikoba ya Mauricio Pochettino huko Chelsea baada ya Muargentina kuachana na miamba hiyo ya Stamford Bridge wiki iliyopita.

Xavi inaelezwa aliambiwa taarifa hizo juzi Ijumaa wakati rais wa klabu hiyo, Joan Laporta alipotembelea mazoezini.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 44 alitangaza Januari kwamba ataachana na Barcelona mwishoni mwa msimu baada ya kichapo kutoka kwa Villarreal kwenye La Liga. Lakini, baadaye iliripotiwa kwamba kocha huyo ataendelea kubaki Nou Camp kabla ya sasa kuibuka taarifa mpya za kufutwa kazi. Na hilo limekuja baada ya Xavi kuweka mambo hadharani kuhusu hali ya kiuchumi ya Barcelona. Xavi, ambaye ni gwiji wa Barcelona alitua kwenye benchi la ufundi la miamba hiyo ya Nou Camp, Novemba 2021.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live