Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Xavi akoshwa na ubora wa Frankie De Jong

Xavi And De Jong Kocha wa FC Barcelona, Xavi Hernandez akimpa maelekezo De Jong

Fri, 21 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa klabu ya Fc Barcelona Xavi Hernandez amemwagia sifa kiungo wa timu yake raia wa Uholanzi Frenkie De Jong kutokana na kiwango alichokionesha katika mchezo wa jana usiku dhidi yas klabu ya Villarreal baada ya ushindi wa goli tatu kwa bila walioupata jana.

Xavi amesifu uwezo aliounesha kiungo huyo katika mchezo wa jana dhidi ya Villarreal mchezaji huyo ambae anahisusishwa kuondoka klabuni hapo kwa muda sasa lakini ameweza kuonesha ubora mkubwa katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Camp Nou usiku wa kuamkia leo.

De jong ambae ameanza michezo miwili mfululizo kwa mara ya kwanza msimu kabla ya kuanza katika mchezo wa jumapili dhidi ya Real Madrid na kupokea kichapo cha magoli matatu kwa moja.

“Alinishawishi kua eneo la kiungo kwenye timu, Alicheza Vizuri na ninamfurahia pia” Alisema Xavi baada ya mchezo wa jana kumalizika Kiungo alikua na kiwango bora sana jana huku akiwa na wastani asilimia 95 kwenye upigaji pasi sahihi huku akifanikiwa kushinda mipira ya chini na juu kwa asilimia 100.

De jong amekua akihusishwa sana kuondoka klabuni hapo lakini kla siku amekua akisimamia msimamo wake anapoulizwa na malengo yake ni kusalia klabuni hapo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live