Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Xavi afunguka ishu Barca

Xavi Kusalia Kama Kocha Wa Barcelona Hadi Juni 2025 Xavi afunguka ishu Barca

Fri, 17 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Barcelona, Xavi amesema mashabiki wa timu hiyo wanatakiwa washikamane na timu na wakubali uhalisia kwa sasa hakuna pesa, hivyo mambo hayawezi kuwa sawa na ilivyokuwa hapo awali.

Miamba hiyo kutoka Catalona, Hispania inapitia kipindi kigumu kwa sasa na ina deni linalofikia Euro 1 bilioni na kulazimika kuuza baadhi ya mali.

Pia iliuza baadhi ya mastaa wake wakubwa akiwamo Lionel Messi na kwa sasa haina tena nguvu ya kushindana sokoni kununua mastaa wakubwa.

Hivi karibuni iliibuka taarifa wanatakiwa kuuza baadhi ya mastaa wa kikosi cha kwanza kwa ajili ya kupata pesa itakazozitumia kufanyia usajili wa dirisha lijalo la sivyo itakuwa ngumu kwao kufanya maboresho.

Xavi amesisitiza, kwa sababu timu haina pesa basi mashabiki wawe wavumilivu wakati benchi la ufundi linajipanga.

Kocha huyu aliyeiwezesha Barca kushinda La Liga na Spanish Super Cup msimu uliopita, mambo yamekuwa magumu msimu huu na hawajapata taji lolote.

Akizungumza na waandishi wa habari Xavi alisema: “Mashabiki lazima waelewe hali yetu ni ngumu sana kushindana kiuchumi, hatupo kama miaka 25 iliyopita na kocha alikuwa anaweza kuja na kusema namtaka yule na huyu akapewa, kwa sasa hakuna hayo mambo, binafsi nimekubaliana na hali hiyo na ndivyo ninavyofanya kazi. Sina maana hatuendi kupambana bali tunahitaji utulivu na muda. Msimu uliopita hatukucheza vizuri sana lakini tulipata ubingwa, msimu huu tumecheza vizuri sana lakini hatukufanikiwa kupata kombe ni baadhi ya vitu vichache tu vimetuangusha.”

Barca ilikuwa ugenini jana kucheza na Almeria katika muendelezo wa La Liga ikiwa ni mchezo wao wa 36.

Chanzo: Mwanaspoti