Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Xavi Simons azitosa Arsenal, man United

Xavi Simons  . Xavi Simons azitosa Arsenal, man United

Tue, 30 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo wa kati wa Paris Saint-Germain Xavi Simons amefanya uamuzi juu ya wapi atacheza kwa msimu ujao na kwa mujibu wa ripoti, amechagua kusalia RB Leipzig kwa msimu mwingine na atasaini mkataba wa mkopo kwa mwaka mmoja zaidi.

Simons mwenye umri wa miaka 21, msimu uliopita alicheza kwa mkopo RB Leipzig na amekuwa akitajwa kwamba anataka kuondoka PSG katika dirisha hili ambapo timu mbalimbali kubwa barani Ulaya ikiwa pamoja na Arsenal, Bayer Munich na Manchester United zinaitamani huduma yake.

Kuna wakati Bayern Munich ilionekana kuwa karibu kumpata staa huyu wa kimataifa wa Uholanzi aliyeonyesha kiwango bora katika michuano ya Euro mwaka huu.

Inaelezwa Bayern ilikubaliana na wawakilishi wa Simons kabla ya kuanza mazungumzo rasmi na mabosi wa PSG ambao hawakufikia muafaka nao.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mwandishi wa Sky Sports, Florian Plettenberg, ni kwamba Simons ambaye msimu uliopita alifunga mabao 10 na kutoa asisti 13, atasaini mkataba mpya wa mkopo wa mwaka mmoja na Leipzig.

“Hakuna uhamisho kwa FC Bayern,” Plettenberg aliandika kwenye X, zamani Twitter, “Pande zote zinazohusika sasa zimefahamishwa kuhusu hilo. Leipzig na Paris wanakamilisha taratibu za mwisho ili Xavi aende tena kwa mkopo kwenye timu hiyo.”

Tajiri wa Man United, Sir Jim Ratcliffe anadaiwa kuwa alishatoa ruhusa ya kusajiliwa kwa staa huyu kama ilivyo kwa mabosi wa Arsenal lakini Simons anaonekana kuwa na furaha zaidi kuendelea kuichezea Leipzig ambako aling’ara msimu uliopita.

Chanzo: Mwanaspoti