Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Xavi Hernandez: Dembélé yupo tayari kwa kazi

Adaembele  Na Xavo.jpeg Dembele akiwa na Xavi

Sat, 4 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Xavi Hernandez ametoa taarifa kuwa mchezaji wake mahiri Ousmane Dembélé kwa sasa kesha pona majeraha yake, na sasa yupo tayari kwa kazi na pia anaweza kuanza siku ya jumamosi dhidi ya Real Betis kama atahitajika.

Dembélé amekosekana miezi minne ya mwanzo kwenye msimu huu, baada ya kufanyiwa oparesheni ya goti, na baada ya kurudi pia akapata mejeraha ya misuli ambayo yalimuweka nje kwa takribani wiki tatu.

Sasa yuko sawa kwa asilimia mia, kesho tutaamua jinsi gani tunataka kucheza, dembele ni mzima, anafuraha na anafanya mazoezi.” amesema Xavi

Barca chini ya Xavi Hernandez wameshinda michezo yao miwili kwenye La Liga, pia wametoa sare dhidi ya Benfica kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya.

Barcelona wanakibarua cha kuwakaribisha Real Betis kwenye dimba lao la Camp Nou, huu ni mchezo wa nne kwa Xavi Hernandez kuingoza tena Barca, na mchezo wa tatu kwenye La Liga tokea achukue mikoba ya kuinoa klabu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live