Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Xavi: Hatustahili kuwepo Ligi ya Mabingwa

Xavi Hernandez Uefa Kocha wa FC Barcelona, Xavi Hernandez

Fri, 14 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa klabu ya Barcelona Xavi amefunguka kua timu yake haistahili kushiriki ligi ya mabingwa ulaya baada ya kushindwa kushinda mchezo wao wa pili baina yao na klabu ya Interzionale Milan usiku wa jana.

Xavi aliyazungumza hayo baada ya mchezo wa juzi usiku dhidi ya Inter Milan ambapo waliponea kufungwa mchezo huo baada ya kusawazisha bao dakika za lala salama kupitia Roberto Lewandowski ndipo kocha wa klabu hiyo akazungumzia anaiona wapi klabu hiyo katika michuano hiyo ya ulaya.

“Kama hutashinda nyumbani dhidi ya Inter Milan basi haustahili kuwepo kwenye mashindao”Sasa hatuitegemei tena, Hatustahili kuwepo kwenye ligi ya mabingwa ulaya. Ni pigo gumu, Gumu sana.” Alisema kocha huyo

“Iwapo mchezaji mmoja au mwingine atafanya makosa, Kama meneja ni jukumu langu. Ninachukua jukumu kamili wachezaji wangu wanapofanya makosa”

“Ilitubidi tuwe makini badala yake tuliingia uwanjani vibaya kipindi cha pili, Lakini bado ni makosa ya kocha” Mbele ya Mashabiki wetu lukuki tulihitajika kuonesha zaidi, Nimesikitishwa na matokeo haya ni ya kikatili mno kwetu” Alieleza Xavi kwa masikitiko makubwa.

Barcelona wameshinda mchezo mmoja tu kwenye kundi lao huku vinara Bayern wakiwa wameshinda michezo yote mpaka sasa huku Inter Milan wakiwa nafasi ya pili na alama zao 7 huku wakihitaji kushinda mchezo mmoja ili kufuzu hatua inayofuata huku Barcelona wakielekea Europa league na wote wakibakiza michezo miwili.

Barca ana kazi kubwa ya kushinda michezo yote huku akiiombea Inter Milan isishinde mchezo mmoja kitu kinachoonekana kua kigumu kwa miamba hao wa Catalan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live