Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Xavi: Hapa ni nyumbani kwa Messi, akaribie wakati wowote

Xavi Hernandez Legend Xavi Hernandez

Mon, 21 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa klabu Barcelona Xavi Hernandez siku ya jumamosi wakati akiwa kwenye kikao na waandishi wa habari alisema kuwa milango iko wazi kwa aliyekuwa nyota wa timu hiyo Lionel Messi kurejea kwenye viunga vya Camp Nuo.

Messi ambaye aliondola kwenye klabu hiyo kwa uhamisho huru, baada ya kushindikana kusaini mkataba mpya kutokana na matatizo ya kifedha ambayo klabu ya Barcelona inapitia.

Xavi alipoulizwa ikiwa milango iko wazi kwa mshambuliaji huyo kurejea alijibu, “Messi ni mchezaji bora wa kihistoria na kwenye historia ya klabu, ana haki ya kurejea na milango iko wazi kwake.

“Ilimradi mimi ni kocha hapa milango iko wazi kwake ikiwa atahitaji kurejea siku yoyote. Messi ni mchezji bora wa kihistoria na kama klabu tunampa heshima kubwa, anayostahili, lakini ana mkataba na PSG, kuna machache naweza kukuambia.

“Ikiwa atahitaji kuja siku yoyote, kuangalia mazoezi, kuzungumza na wakufunzi, milango iko wazi kwa sababu ni mchezaji bora wa kihistoria kwenye klabu hii.”

Tokea Messi aondoke klabu ya Barcelona haikuwa na muendelezo mzuri, mpaka alipochaguliwa Xavi kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo, ndio alieleta matumaini mapya kwenye klabu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live