Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Xavi Amekataa kazi lakini anaishi kishua

Xavi Kishua Xavi Amekataa kazi lakini anaishi kishua

Mon, 2 Sep 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kuachana na Barcelona mwisho wa msimu uliopita, Xavi Hernandez anadaiwa kuwa alisamehe karibia Euro 12 milioni iliyokuwa ni pesa ya mshahara pamoja na haki za matangazo ya picha yake.

Mbali ya kusamahe kiasi hicho cha pesa Xavi aliachana na ofa kutoka timu mbalimbali zilizoonyesha nia ya kutaka kumwajiri katika dirisha lililopita licha ya kuwekewa ofa nzuri zaidi ya ile ambayo alikuwa akiipokea Barcelona.

Staa huyu wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania anadaiwa kufanya yote hayo kwa sababu pesa kwake sio shida kwa sababu ana utajiri wa kutosha.

ANAPIGAJE PESA?

Anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Dola 65 milioni ambao unatokana na mjumuisho wa mali alizonazo na pesa alizokuwa anapata akiwa kocha wa Al-Sadd ya Qatar na Barcelona.

Mbali ya mshahara aliokuwa anaupata, Xavi ameendelea kujiingiza pesa kupitia madili mengine nje ya uwanja ambapo kwa sasa anahudumu kama balozi wa kampuni ya Audi Qatar, ambayo ni tawi la kampuni ya uzalishaji wa magari ya Audi kutoka Ujerumani.

Pia anakunja mkwanja wa kutosha kupitia mkataba wake wa ubalozi na Adidas, Danet, Garmin, Gillette na QNB.

Mhispania huyu pia alishawahi kuwa balozi wa kampeni ya FIFA kwa kushirikiana na CAF iliyoitwa “11 against Ebola” ambapo kazi yake kubwa ilikuwa ni kuelemisha jamii juu ya ugonjwa huo hatari wa Ebola.

MSAADA KWA JAMII

Mwaka 2011 alitoa Euro 100,000 kwenda taasisi ya ICRC ili kusapoti ununuaji wa baadhi ya vifaa kwa ajili ya mashirika ya msalaba mwekundu yaliyokuwa yanafanya kazi huko nchini Afghanistan.

Pia aliwahi kutoa boti yake kwenda kwa shirika lisilo la kiserikali la Proactive Open Arms ili litumike kusaidia kuokoa wakimbizi waliokuwa wanatumia bahari kuingia Ulaya. Boti hiyo ilisaidia zaidi ya wakimbizi 3,000 waliokuwa kwenye hatari ya kuzama baharini.

MAGARI ANAYOMILIKI

-Audi Q5 -Dola 54,800

-Q7 Luxury Edition-Dola 85,000

-Ferrari 458 Italia- Dola 474,980

-BMW Z4- Dola 75,000

MJENGO

Ana bonge la jumba huko Barcelona, Hispania ambalo lina kadiriwa kuwa na thamani ya Pauni 5 milioni. Nyumba hiyo ndani yake kuna bwawa la kuogelea, sehemu kwa ajili ya kusomea vitabu na sehemu nyingine kwa ajili ya michezo mbalimbali.

MAISHA NA BATA

Anapopata muda wa kupumzika jamaa huwa anakula bata sana na hiyo ilisababisha hata aamue kununua boti yake binafsi ili aponde raha vizuri.

Tangu mwaka 2013, Xavi yupo kwenye ndoa na Nuria Cunillera ambaye hadi sasa amezaa naye watoto wawili ambao mmoja alizaliwa mwaka 2016 na mwingine mwaka 2018.

Chanzo: Mwanaspoti