Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wydad yaweka mkwanja mrefu kwa Mzize

Clement Mzize Clementinho Wydad yaweka mkwanja mrefu kwa Mzize

Thu, 15 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Wydad inaandaa dau jipya na kubwa zaidi kwa Clement Mzize licha ya Yanga kuwaambia hawana mpango wa kumuuza nyota huyo.

Duru za habari nchini Morocco ziliulizia upatikanaji wa nyota huyo ikiwemo kumfuata mchezaji mwenyewe ambaye aliwaambia wakazungumze na Klabu kwa sababu ana mkataba na vibopa wa Yanga waliwajibu kiufupi kuwa Mzize hauzwi kwa sasa.

Yanga wanaamini nyota huyo atakuwa ni muhimu kwa muda mrefu kama ambavyo Wydad wanaamini kitu kwa nyota huyo na sasa baada ya kuambiwa hauzwi Wydad wanatarajia kupeleka ofa rasmi kubwa kuliko waliyojipanga nayo wakati wa maulizo ya upatikanaji wake.

Katika hatua nyingine klabu hiyo imeulizia upatikanaji wa nyota wa Azam FC Jhonier Blanco na Yeison Fuentes na wanasubiri majibu ya Azam FC kwa nyota hao. Wydad wanataka kutengeneza timu mpya baada ya kizazi cha mafanikio kuzidiwa msimu uliopita!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: