Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wydad yawarudisha watovu wa nidhamu kikosini kuimaliza Simba SC

Said Naciri Rais wa Wydad Casablanca Said Nacir

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Wydad Casablanca Said Nacir sasa amepagawa anahaha kila namna timu yake iwafunge Simba.Na anawajua Simba karibuni hawana hofu dhidi yao.

Wachezaji wawili walio nje ya timu kwa muda mrefu wamerejeshwa Zuhair Al-Mutaraji na Ismail Al-Mutaraji na wameshaanza mazoezi ya kumvaa mnyama.

Baada ya timu kurudi kutoka Ivory Coast Rais Said Naciri alifanya kikao kuwarudisha watovu wa nidhamu kuja kusaidia timu.

Maamuzi haya ni baada ya mashabiki kumuashia moto Rais wa klabu kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kuwabania vijana hao ambao kosa lao lilikuwa kuwa na mgomo baridi wa kudai bonus na maslahi yake mengine lakini Rais huyo hakutaka pia kuwauza januari

Lakini nyota Zuhair Al Mutaraj mapema kabisa alishapishana na kocha Adel Ramzi na akasema hayupo kwenye mipango yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live